Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



ATHARI ZA VITA KWA WATOTO
Namba: 249982 Tarehe: 1390/00/00Rejea: print

ATHARI ZA VITA KWA WATOTO


 ATHARI ZA VITA KWA WATOTO

ATHARI ZA VITA KWA WATOTO

Mamilioni ya watoto huko Colombia, Iraq, Afghanistan, Uganda, Darfur Sudan, Sierra Leone na katika maeneo mengine

mengi kunakojiri vita duniani wameuawa, kujeruhiwa, kupoteza wazazi na jamaa zao na kulazimika kuishi makambini. Ni

wazi kuwa asilimia 95 ya wahanga wa migogoro ya kivita ni raia, huku zaidi ya asilimia 80 wakiwa ni watoto na

wanawake. Kitendo cha watoto hao kutengana au kuwa mbali na famila zao au kuwa mayatima, kumewalazimisha baadhi yao

kubeba jukumu la kuwalea wadogo zao au jamaa zao wakiwa na umri mdogo. Aidha watoto hao hukumbwa na matatizo

mbalimbali kama vile kutopata chakula cha kutosha, maji safi na salama, elimu, huduma za afya na usalama. Zaidi ya

hayo, watoto wanaoishi kwenye maeneo ya vita wanaingizwa kwenye migogoro ya kivita kama wafuasi wa serikali na

makundi yanayobeba silaha. Baadhi ya watoto hulazimishwa kujiunga na jeshi na wengine wakijunga kwa khiari yao ili

kuepuka umaskini au ikiwa ni katika kutafuta usalama, wakiogopa machafuko ya vita na kuwa wakimbizi. Vijana

wasiopungua elfu 30 walio na umri wa chini ya miaka 18 wengine wakiwa wadogo sana katika umri wa miaka minane, hivi

sasa wanahudumu kama askari katika nchi 30 duniani. Watoto hao wa kike na wa kiume wanatumiwa jeshini kama wapagazi,

wapishi na wahudumu wa kazi nyingine jeshini. Takwimu zinaonyesha kuwa watoto wa kike mara nyingi hutumiwa kama

watumwa wa ngono na kuolewa kwa nguvu na makamanda wa jeshi. Baadhi yao hujiingiza kwenye ngono haramu ili kupata

mahitaji kama vile chakula, fedha na ulinzi. Hatari ya maambukizo ya HIV na ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa ni

ya kiwango cha juu katika maeneo ya vita. Watoto wanaotumiwa kama askari katika nchi zilizokubwa na vita na

machafuko siku zote huathiriwa vibaya kiakili na kimwili, na suala hilo huwachochea kutenda vitendo viovu na vya

kikatili. Kwa hiyo madhara yanayowasibu watoto hao huwa ni makubwa. Huku wakiwa wameathirika na kumbukumbu chungu za

vita, watoto wengi huendelea kusumbuliwa na majinamizi na kumbukumbu za mateso na udhalilishaji wa kijinsia

waliofanyiwa, au kushuhudia, au kulazimishwa kuufanya wakati wa vita. Kwani baadhi ya watoto waliokuwa wakitumiwa

kama askari vitani huko nyuma, huogopa kurejea katika jamii, kwa sababu wenyeji waliwashuhudia wakitenda jinai

mbalimbali. Katika maeneo ya vita mtoto wa kike huwa hana usalama. Taathira za kimwili na kinafsi za mtoto huyo

huongezeka mara kwa mara kutokana na aibu na kukataliwa na jamii. Kwa hiyo, mtoto wa aina hiyo anahitaji uangalizi

maalumu. Athari kubwa zaidi humpata mtoto wakati wazazi wanapouawa, kujeruhiwa, kutishwa au wanaposhindwa kutekeleza

majukumu yao, na pale mtoto anaposhuhudia mzazi wake akifanyiwa vitendo vya kikatili au akishiriki katika kuwadhuru

wengine.

Vita hudhoofisha misingi mikuu ya maisha ya watoto, huharibu makazi yao na kuvunjilia mbali matumaini yao ya

baadaye. Kwa upande wa athari za kinafsi au kiakili na kisaikolojia, watoto hao hukumbwa na matatizo yafuatayo: huwa

na hali ya mfadhaiko, huzuni, baadhi yao huwa wakatili, wengine hukumbwa na hali ya woga na wasiwasi. Bbaadhi ya

watoto hao huota ndoto mbaya nyakati za usiku na (mara zote hudhani kuwa wako vitani), hukosa uchangamfu, baadhi yao

huwa na tabia ya kulia. Hupatwa na hasira za mara kwa mara na wengine hujikojolea nyakati za usiku na hupenda

kuchukua maamuzi ya haraka n.k. Kwa upande wa athari za kimwili, watoto katika maeneo yenye migogoro ya vita

hukumbwa na matatizo yafuatayo: hupata ulemavu unaosababishwa na kujeruhiwa na risasi au mabomu ya kutegwa ardhini

na milipuko mingine ya mabomu, hupata mimba haramu za utotoni, na hata kukumbwa na magonjwa mengine ya zinaa na

ukimwi. hujiingiza katika utumiaji madawa ya kulevya na unywaji pombe na vileo, ukahaba n.k. Kuhusu kuheshimiwa haki

za mtoto, Shirika la Msamaha Duniani limetoa maazimio kadhaa likizitolea mwito serikali, makundi ya upinzani na wale

wote wanaowatumia vibaya watoto kuheshimu sheria zifuatazo. Mosi:Kuhakikisha kuwa watoto walioko katika seli au jela

au wale wanaolelewa katika taasisi za serikali au watu binafsi wanalindwa na aina zote za unyanyasaji na mateso,

vitendo visivyo vya kibinadamu au adhabu zisizostahili. Pili, Watoto wanaofikishwa mbele ya sheria kwa makosa

waliyoyatenda wanapaswa kuadhibiwa kulingana na sheria za kimataifa. Nchi mbalimbali zinapaswa kupiga marufuku

adhabu ya kifo kwa yule aliye chini ya umri wa miaka 18. Watoto ambao wamekuwa wahanga wa haki za binadamu na

kufanyiwa mateso wanapasa kulipwa fidia itakayowawezesha kupewa huduma na matibabu ili ajiunge na tena jamii. Tano,

watoto wote wanapaswa kufungwa jela katika hatua ya mwisho kabisa na kwa muda mfupi, ripoti zote zinazohusiana na

mauji na ukiukaji mwingine wa haki za watoto ni lazima zichunguzwe kwa kina, kuzuia kuwaingiza watoto walio naumri

chini ya miaka 18 katika majeshi ya serikali na makundi hasimu yanayobeba silaha n.k.

Je Umoja wa Mataifa una mchango gani na unapaswa kufanya nini kuhusiana na masaibu hayo yanayowakumba watoto katika

maeneo yenye vita? Unapaswa kupunguza hatari zinazowakabili watoto kwa kusambaza suhula mbalimbali katika maeneo

yanayokumbwa na vita, kuwasaidia watoto waliohamishiwa kwenye makambi ya wakimbizi, kuanzisha mipango ya kuwahudumia

watoto hao walioathirika mara baada ya kurejea nyumbani wakiwa salama ikiwa n pamoja na kuwatibu maradhi

waliyoyapata vitani yakiwemo ya kiakili na kinafsi. Uunapaswa pia kuandaa utangulizi wa kuwaingiza mashuleni watoto

wao, vile vile unapaswa kuzisaidia kifedha taasisi zisizo za kiserikali ili ziweze kushirikiana na vyombo vya habari

kutangaza na kuweka wazi matatizo yanayowakabili watoto katika maeneo yaliyokumbwa na vita. Na mwisho Baraza la

Usalama la Umoja wa Mataifa litekeleza jukumu lake kuu la kuwalinda watoto wakati wa kujiri vita na na machafuko.

Ni hayo tu kwa leo.

 

 

 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani