Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Malaysia, mwenyeji wa kikao cha pili cha kimataifa cha utafiti wa Qur'ani
Namba: 273022 Tarehe: 1390/00/00Rejea: iprint

Malaysia, mwenyeji wa kikao cha pili cha kimataifa cha utafiti wa Qur'ani

Kikao cha pili cha kimatifa cha utafiti wa Qur'ani kimepangwa kufanyika Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia tarehe 22 na 23 Februari mwakani. 

 Malaysia, mwenyeji wa kikao cha pili cha kimataifa cha utafiti wa Qur

Kikao hicho ambacho kimeandaliwa na Kituo cha Utafiti wa Qur'ani na Kundi la Utafiti wa Qur'ani na Hadithi la Chuo Kikuu Cha Malaysia kitafanyika katika ukumbi wa chuo hicho. Waandaaji wa kikao hicho wamealika mashirika, jumuiya na makundi yote yanayojishughulisha na masuala ya Qur'ani Tukufu na Hadithi za Mtume (saw) kushiriki kwenye kikao hicho cha kimataifa.

Kikao hicho kitajadili masuala mbalimbali yanayohusiana na Qur'ani pamoja na Hadithi yakiwemo ya tafsiri ya Qur'ani, sheria za Kiislamu, miujiza ya Qur'ani, kutumiwa elimu na teknolojia ya kisasa katika kuhudumia Qur'ani na mbinu zinazopasa kutumiwa kwa ajili ya kukiarifisha kitabi hicho kitakatifu cha Mwenyezi Mungu.

Badhi ya malengo ya kuandaliwa kikao hicho yametajwa kuwa ni kuunganisha taasisi na mashirika yanayoshughulikia masuala ya Qur'ani, kuchunguza utafiti ambao umefanyika kuhusiana na Qur'ani, kuwatambulisha watu mashuhuri wanaohudumia Qur'ani na kutumia teknolojia ya kisasa katika kueneza mafundisho ya Qur'ani.
 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani