Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Gaddafi auawa na makombora ya NATO alipokuwa akijaribu kutoroka
Namba: 273262 Tarehe: 1390/00/00Rejea: tehranprint

Gaddafi auawa na makombora ya NATO alipokuwa akijaribu kutoroka

Habari kutoka Libya zinasema kuwa dikteta wa Libya Kanali Muammar Gaddafi amefariki dunia baada ya kujeruhiwa vibaya kichwani na miguuni alipokuwa akijaribu kutoroka kutoka mji wa Sirte 

 Gaddafi auawa na makombora ya NATO alipokuwa akijaribu kutoroka
Habari kutoka Libya zinasema kuwa dikteta wa Libya Kanali Muammar Gaddafi amefariki dunia baada ya kujeruhiwa vibaya kichwani na miguuni alipokuwa akijaribu kutoroka kutoka mji wa Sirte. Habari zaidi zinasema kuwa Gaddafi akiwa kwenye msafara mkubwa wa magari alijaribu kutoroka punde baada ya wanamapinduzi wa Libya kuutwaa kikamilifu mji wa Sirte mapema leo. Baadaye ndege za kivita za NATO ziliufuata msafara huo na kuudondoshea mabomu ambapo Gaddafi alijeruhiwa vibaya kichwani na miguuni. Imeripotiwa kuwa wapiganaji wanamapinduzi walimkamata Gaddafi akiwa hai lakini akafariki baadaye kutokana na majeraha. Video inayowaonyesha wanamapinduzi wakiuburuza mwili wa Gaddafi imeenea katika kanali za televisheni na kwenye intaneti. Kamanda wa ngazi za juu wa jeshi la wanamapinduzi Abdel Majid Mlegta amethibitisha kufariki dunia kanali Gaddafi na kusema kuwa ushahidi wa picha na video umetolewa hadharani. Msemaji wa Baraza la Mpito la Libya Abdel Hafez Ghoga pia amethibitisha kuuawa Gaddafi.
 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani