| Namba: 296289 | Tarehe: 1390/00/00 | Rejea: | print |
Miaka 33 ya Mapinduzi ya kiislamu ya Iran Ismail Hania, kuonana na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran |
Ismail Hania, Waziri Mkuu Palestina ameonana na Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya
Ayatullah Khamenei amesisitiza katika mazungumzo hayo kwamba uungaji mkono wa mataifa ya dunia hasa umma wa Kiislamu kwa mapambano ya Kiislamu ya Palesstina ni stratijia ya hali ya juu sana ya makundi ya Kiislamu, na kuongeza kuwa: Ushindi uliopatikana katika miaka ya hivi karibuni huko Palestina na hata sehemu ya sababu za kujitokeza mwamko wa hivi sasa wa Kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika ni katika matunda matukufu ya muqawama na kusimama kidete wananchi na makundi ya Kiislamu ya Palestina mbele ya mashinikizo makubwa ya maadui.
Ameongeza kuwa, ushindi wa siku za usoni pia ambao utapelekea kushuhudiwa ahadi ya Mwenyezi Mungu (ya kuwanusuru wanaoinusuru dini Yake) utapatikana pia chini ya kivuli hicho hicho cha muqawama na kusimama imara mbele ya maadui.
Aidha ameashiria suala la kusimama kidete wananchi wa Ghaza na kushindwa utawala wa Kizayuni wa Israel katika masambulizi yake ya siku 22 kwenye ukanda huo na kuongeza kuwa: Hapana shaka hata kidogo kwamba hisia kali zilizokuwa zimerundikana muda mrefu kati ya wananchi wa nchi za eneo hili kuhusiana na kadhia ya Ghaza zimechanga katika suala zima la kuripuka ghafla moja na kwa sura ya ajabu eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Ayatullah Khamenei amemukhutubu Bw. Ismail Hania, Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina akimwambia: Sisi hatuna shaka hata kidogo katika suala zima la msimamo wako wa kutotetereka pamoja na ndugu wengine wanamuqawama, na wananchi wa Palestina nao hawawezi kutarajia kitu kingine ghairi ya hicho kutoka kwa harakati ya muqawama wa Kiislamu ya Palestina.
Aidha amekumbushia hatima iliyomfika Yasir Arafat, (Kiongozi wa zamani wa PLO) ambaye wananchi Waisalmu wa eneo hili yalimtoa kwenye itibari baada ya kutoka katika njia ya muqawama licha ya kwamba alipendwa sana katika miaka ya awali ya mapambano ya ukombozi wa Palestina na kuongeza kuwa: Muqawama na kusimama kidete ni mambo yanayoandaa mazingira ya kuvutika nyoyo za watu na hiyo ni hazina kubwa sana ambayo inabidi ilindwe wakati wote.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran amesisitiza pia juu ya msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kuihesabu kadhia ya Palestina kuwa ni kadhia ya Kiislamu na kuliona suala la Palestina kuwa halina tofauti na masuala mengine ya taifa la Iran na kuongeza kuwa, Iran imesimama imara na itaendelea kusimama imara katika kadhia ya Palestina na daima itaendelea kuwa pamoja na wananchi wa taifa hilo na muqawama wao.
Kwa upande wake, Bw. Ismail Hania, Waziri Mkuu wa serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ya Palestina ameelezea kufurahishwa kwake mno na fursa aliyopata ya kuonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na sambamba na kutoa mkono wa baraka na fanaka kwa mnasaba wa maadhimisho ya miaka 33 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema: Maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka huu yamefanyika katika hali ambayo dunia na eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika likiwa linaendelea kushuhudia mabadiliko makubwa hasa yanayotokana na mwamko wa Kiislamu.
Vile vile ameishukuru serikali na taifa la Iran kwa uungaji mkono wake mkubwa kwa kadhia ya Palestina na ameongeza kwa kusema: "Mimi jana niliona kwa karibu, na pia wakati nilipopaa kwenye helikopta nilishuhudia kwa macho yangu jinsi mamilioni ya watu wa Tehran walivyoshiriki kwenye maadhimisho ya Bahman 22 (Februari 11, siku zinapofikia kileleni sherehe za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran) na sisi tunalihesabu taifa la Iran kuwa ni hazina ya kiistratijia kwa ajili ya suala la Palestina."
Baada ya hapo Bw. Ismail Hania ameashiria stratijia tatu za serikali halali ya Palastina na kufafanua mikakati hiyo akisema: "Kukomboa ardhi zote za Palestina kuanzia baharini hadi mtoni, kushikamana na muqawama na kutokubali mazungumzo yasiyo na maana pamoja na kuhakikisha kuwa kadhia ya Palestina inaendelea kuwa na sura ya Kiislamu na inaendelea kushikamana na Uislamu ndizo stratijia zetu tatu kuu."
Waziri Mkuu wa serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ya Palesina vile vile amesisitiza juu wa wajibu wa kuwa na imani na ahadi ya Mwenyezi Mungu pamoja na kuwa na yakini kikamilifu kwamba taifa la Palestina hatimaye litashinda tu na utawala wa Kizayuni mwishowe utaangamizwa tu.
Aidha amemwambia Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwamba: Kama ambavyo umesema hivi karibuni, sisi (Waislamu) kamwe hatuko tena zama za "