| Namba: 322499 | Tarehe: 2012/06/16 - 10:09 | Rejea: abna | print |
Ripoti ya ABNA- Sheikh Ali Ibn Abdisamad alisema: Imepokelewa katika Vitabu kuwa kipindi ambacho Haruna Rashid alidhamiria kumuuwa Imam Musa Ibn Jaafar alielekea kwa Fadhl Ibn Rabii na kumwabia nataka unifanyie kazi moja na ujira wake ni Dirham Alfu moja , Fadhl Ibn Rabii alisema; ni jambo gani hilo?! Haruna Rashid akamwambia: suala lillilokuwa hapa ni kumuuwa Imam Musa Ibn Jaafar(as), Fadhl Ibn Rabii Akasema: hakuna neno.
Fadhl Ibn Rabii anasema: nilipokwenda Nyumbani kwa Imam Kadhim nilimkuta yupo katika Swala na nikasubiri amalize Swala yake na baada ya kumaliza Swala Imam(as) aliniangalia huku akitabasamu kwa kusema; na tambua nini kilichokulea tafadhali nakuomba ni Swali rakaa mbili, Fadhl akampa muda, Imam(as) kwa mara nyingne akaenda kuchukua udhu na akaswali rakaa mbili kwa unyenyekevu, baada ya hapo nilishindwa nini cha kufanya kwani hali alokuwa nayo Imam ilifanya niondoke haraka na kumuelezea kisa hicho Haruna Rashid, Haruna Rashid Alishikwa na kilio na kusema Eee! Mola ni samehe.
Haruna Rashid alishidwa nini cha kufanya ila alitoa amri ya kumfunga Imam Musa Al-Kadhim(as) na kutuma watu tofauti wamuudhi Imam Musa Al-Kadhim(as).
Baada ya kifungo na mateso ya hapa na pale hatimae Imam Musa Al-Kadhim(as) alipewa sumu katika chakula chake na kuwa sababu ya kifo chake.