Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Waziri mkuu wa Italia azuru nchi kadhaa
Namba: 333090 Tarehe: 2012/07/30 - 19:10Rejea: ABNA.irprint

Mwaka 2012 ni mwaka mporomoko wa kiuchumi Ulaya
Waziri mkuu wa Italia azuru nchi kadhaa

Waziri mkuu wa serikali ya Italia Mario Monti anataraji kuelekea jiji Madrid nchini Uhispania kukutana na mwenzie Mariano Rajoy wakati nchi hiyo nayo ikikabiliwa na tatizo la mdororo wa uchumi katika ukanda wa nchi zinazo tumia sarafu ya Ulaya.
 

 Waziri mkuu wa Italia azuru nchi kadhaa

Viongozi hao wawili watakutana kwa mazungumzo na kufanya kazi kwa pamoja kabla ya kuendesha mkutano na vyombo vya habari. Waziri mkuu wa Italia atakutana pia na mfalme Juan Carlos.

Waziri mkuu Mario Monti, kabla ya kuzuru Uhispania, ataelekea pia jijini Paris siku ya Jumanne ambako atakutana na rais wa Ufaransa Francois Hollande na siku ya Jumatano na alhamisi atatembelea nchini Finlande katika mazungumzo na mwenziwe Jyrki Katainen.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameyahakikishia masoko ya Umoja huo kuhusu juhudi wanazo zifanya kuhakikisha uchumi wa nchi wanachama unaimarika na hivo kuepuka mporomoko wa kiuchumi.

Ujerumani na Italia zimekubaliana kufanya jitihada ziwezekanazo ili kulinda uchumi wa ukanda wa Euro.

 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani