| Namba: 333423 | Tarehe: 2012/07/31 - 22:31 | Rejea: ABNA.ir | print |
Siku ya Wanawake barani Afrika |
Wanawake lakini wamekuwa wa kwanza katika mataifa kadhaa ya Afrika kukumbana na matatizo kadhaa, hasa katika maeneo ya vita. Waandishi wa habari waamezungumza na mmoja wa wanaharakati anayefanyakazi katika shirika la kijamii linalopigania amani katika eneo la mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Janine Mbandu , na alitaka kujua siku hii ina umuhimu gani kwa mwanamke wa eneo hilo, alijibu kuwa: Siku hii ni siku adhimu Ulimwenguni kwani siku hii lazima Wanawake wafahamu umuhimu wake, siku ya Wanawake Duniani ni siku ya kuonyesha kuwa Wanawake wanahaki ya kufanya kazi kwa matakwa yao na sikufanyishwa kazi kwa nguvu km wanavyofanyiwa katika baadhi ya Nchi, aidha Wanawake wafahamu kuwa ni siku ya kuonyesha umahiri wao katika uchapakazi na kuonyesha kuwa Wanawake sio chombo cha biashara kama wanavyo jivulia heshima baadhi ya Wanawake Duniani.