| Namba: 334141 | Tarehe: 2012/08/03 - 22:42 | Rejea: abna.ir | print |
Ghadhabu za magharibi dhidi ya Uislamu kudhihirishwa Shirika la Google na Facebook kufunga ukurrasa wa Televisheni ya Al-Manar |
Ripoti ya shirika la habri la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Imearifu kuwa: Shirika la Google, Apple na Facebook kufunga na kufuta ukurasa wa Televisheni ya Hizbullah Al-Manar, na bila kutajwa sababu za ufungaji wa Televisheni hiyo hadi sasa.
Televisheni ya Al-Manar ilianza kurusha matangazo yake katika Mtandao wa Google+ , na Google baada ya kuona hivyo ilifunga haraka matangazo ya Televisheni hiyo, aidha Simu za shirika la Apple katika masaa 48 yalopita ilifunga Televisheni hiyo.
Abraham Fox Man alisema: Kufungwa Televisheni ya Al-Manar ni kuwa Televisheni hiyo ipo kinyume na Israel.
Viongozi wa Televisheni hiyo walisema: Kufungwa Televisheni ya Al-Manar ni jambo lilosubiriwa muda mrefu kwani pigo walopigwa wa Israel katika Vita ya Siku 33 mwaka 2006 kamwe hatosahau, na kufunga Televisheni hiyo katika Internet ni moja kati ya kutoa majungu na maumivu walokuwa nayo.
Akiendelea kusema: Nchi za Kimagharibi hudai Demokrasia ila Nchi hizo haziwezi kuvumilia na kustahamili Televisheni ya Al-Manar.
Akimalizia kwa kusema: Televisheni ya Al-Manar Amerika yahesabiwa kama Televisheni ya Magaidi na pigwa marufuku Nchini humi mwaka 2004, Ufaransa na Danmark pia walifunga Televisheni hiyo katika baadhi ya Satellite za Ulaya.