| Namba: 336112 | Tarehe: 2012/08/11 - 17:57 | Rejea: abna.ir | print |
Jeshi la Syria kusafisha Kijiji cha Aleppo |
Jeshi la Serikali limefanikiwa kuchukua utawala wa eneo la Salaheddin ambalo lilikuwa linashikiliwa na Wapiganaji wa Waasi baada ya kutokea mapigano makali ya kutaka kukomboa eneo hilo lililokua linashikiliwa na Jeshi Huru la Syria.
Wapiganaji wa Jeshi Huru la Syria wamekiri kurudishwa nyuma baada ya kuzidiwa nguvu kwenye mashambulizi ambayo yamefanywa na Wanajeshi wa Jeshi la Serikali waliojiapiza kuwasambaratisha Waasi hao.
Jeshi Huru la Syria limesema kwa sasa linajipanga upya na hawawezi kukata taama baada ya kuupoteza Mji wa Salaheddin na badala yake watafanya mashambulizi kuhakikisha wanaukomboa kutoka mikono ya serikali.
Wapiganaji hao wa Jeshi Huru la Syria wamekiri kwa sasa wanakabiliwa na upungufu wa silaha na hivyo wameanza kuomba msaada ili waweze kutimiza lengo lao la kupambana klikamilifu na Jeshi la Serikali.
Haya yanakuja wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa UN ukielezwa kumteua Mwanadiplomasia Lakhdar Brahimi raia wa Algeria kuchukua nafasi ya Kofi Annan kwenye kupatanisha mgogoro wa Syria uliodumu kwa miezi kumi na saba sasa bila ya suluhu.