| Namba: 336337 | Tarehe: 2012/08/12 - 18:34 | Rejea: abna.ir | print |
Waziri wa Afya atahadharisha kutokea magonjwa baada ya Tetemeko la Ardhi |
Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Dr.Mardhiya Wahid Dastjordi Waziri wa Afya wa Iran alieleza kuwa; Mahitaji muhimu kutokana na tetemeko la Ardhi Tabriz kaskazini magharibi mwa Iran yaendelea na Madaktari wafanya kazi usiku na mchana ili kuweka mazingira safi na kusaidia watu walokubwa na janga hilo.
Aidha alisema: Tatizo kuwba ni kukatika Maji na Umeme katika Vjiji hivyo, ukatikaji wa Maji ni hatari kwa Afya ya watu wa Vijiji hivyo kwani watalazimika kutumia Maji yasokuwa salama na hii itasababisha kuleta magonjwa na maradhi hatari.
Waziri huyo alihudhuria sehemu hizo ili kutathmini na kuwapa salam za rambi rambi kwa wafiwa wa sehemu hizo, na baada ya kuona mazingira ya Kijiji kimoja alisema: %80 ya Kijiji hiki kunatatizo la Maji na hii ni hatari kwa Kijiji lazima kufikishwe huduma ya Maji haraka iwezekavyo.
Akimalizia kwa kusema: la kusikitisha ni kwamba Hospitali ya Ahar na Haris imeharibika vibaya na haiwezi kupokea majeruhi na hapa karibu hakuna Hospitali.