Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Hilary Clinton ameeleza hayo wakati alipoongea kwa simu na waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergei Lavrov. Bw. Lavrov amesisitiza kuwa, mgogoro wa Syria unapaswa kutatuliwa kwa njia ya amani na mazungumzo, pamoja na juhudi za muda mrefu za pande zote, kama ilivyofanyika wakati wa kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Yemen.
Wizara ya mambo ya nje ya Russia imesema, Russia inalaani vikali mauaji yaliyotokea hivi karibuni huko Houla nchini Syria, lakini haikubaliani na azimio la Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji hayo, kwani linawakilisha maoni ya Baraza hilo pekee. Russia ina wasiwasi kuwa, mauaji hayo yanatumiwa na baadhi ya nchi kuhujumu mpango wa amani uliopendekezwa na mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu kuhusu mgogoro wa Syria Bw Kofi Annan