| Namba: 323171 | Tarehe: 2012/06/19 - 08:58 | Rejea: | print |
Maendeleo TZ Tanzania yagundua malimbikizo ya gesi asilia |
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki iliyopita huko Dodoma na waziri wa nishati na madini wa Tanzania Sospiter Muhongo, aidha amesema mbali ya kiwango hicho pia kimegunduliwa kisima cha gesi kiitwacho Lavani. Ugunduzi huo umefanywa na kampuni ya Statoil and Exxon Mobil ya Norway kilomita 80 kutoka pwani ya mkoa wa Lindi. Waziri huyo pia amesema kwa miaka mitatu iliyopita shughuli za utafutaji wa gesi na mafuta zimekuwa zikifanyika ambapo juhudi zilikuwa zikielekezwa zaidi katika maeneo ya kina cha bahari ya Hindi.