Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Polisi nchini Tanzania kumshika mkenya mmoja aliemteka Daktari nyara
Namba: 329061 Tarehe: 2012/07/14 - 19:01Rejea: ABNA.irprint

Polisi nchini Tanzania kumshika mkenya mmoja aliemteka Daktari nyara

Jeshi la polisi nchini Tanzania linamshikilia raia mmoja wa kenya ambaye anatuhumiwa kuhusika na utekaji nyara na kumtesa kiongozi wa chama cha madaktari Ulimboka steven ambaye alitekwa kuteswa na kutupwa nje kidogo ya jiji la Dar es salaam mnamo mwezi wa sita mwaka huu. 

 Polisi nchini Tanzania kumshika mkenya mmoja aliemteka Daktari nyara

Kamanda wa polisi mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova amemtaja Joshua Gitu Mhindi mwenye umri wa miaka 31 na kuongeza kuwa amekutwa na hati ya kusafiria inayothibitisha uraia wa mtu huyo ambaye tayari jalada la kesi yake limekabidhiwa kwa mwendesha mashtaka wa serikali ya Tanzania.

Kiongozi wa chama cha madaktari nchini Tanzania alitekwa nyara,kuteswa na kutupwa nje kidogo ya jiji la Dar es salaam mwezi wa sita na watu ambao hawakufahamika,na kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu nje ya Tanzania.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi nchini humo limepiga maandamano ya madaktari yaliyopangwa kufanyika siku ya jumatatu 16 mwezi huu.

 




Barua pepe:
Jina:
Ujumbe:
Enter security code
erfan
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani