| Namba: 332080 | Tarehe: 2012/07/26 - 22:18 | Rejea: ABNA.ir | print |
Mazayuni wateketezwa Tende za Israel kupigwa marufuku Uingereza |
Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt (as)-ABNA- Inaeleza kuwa; Baadhi ya Taasisi za Kiisrael Nchini Uingereza zimeomba Nchi za Ulaya kuiwekea Israel vikwazo vya kiuchumi kama walivyo zuiya Tende za Israel kuingizwa Uingereza, lengo maombi hayo ni kwa kile walichoeleza kuwa; Nchi ya Israel ya jenga Majumba katika Ardhi ya Palestina kwa nguvu na ujengaji huo upo kinyume ya Sheria na kanuni za Kimataifa.
Vikundi na Taasisi hizo zimetaka Nchi za Ulaya na Taasisi tufauti kuungana nao kwa kuiwekea vikwazo Israel na kutaka Waislamu kujiunga na Taasisi hizo kuto nunua bidhaa aina yoyote ya Israel.
Aidha kabla ya hapo bidhaa za Israel zilipigwa marufuku katika baadhi ya Maduka ya Ulaya.
Kufika Mwezi wa Mtukufu wa Ramadhani Israel iliongeza idadi ya uzalishaji na uagizaji wa Tende katika Bara la Ulaya kwani Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Waislamu hutumia Tende zaidi kuliko Miezi mingine, kwa sababu hiyo Israel iliongeza Idadi ya uagizaji wa Tende Barani mara Kumi kwa kutaka faida zaidi ila Waislamu na baadhi ya Nchi za Ulaya ziligundua hilo na kupinga uagizaji wa Tende kiholela holela.
La kuzingatia ni kwamba Nchi ya Israel kwa Mwaka huzalisha Tani 100 na 15% huagizwa Bara la Ulaya.