Mwanzo    Nyumbani    Links   Kurasa ya kijani    Tafuta  



Habari Muhimu
- Habari Muhimu



Hukumu dhidi ya haki za binadamu
Ujumbe wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt(as) katika kuomba baadhi kunyongwa Sheikh Namer
Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt(as) imeomba Taasisi na Jumuiya za Kimataifa za haki za binadamu ulimwenguni haraka iwezekanavyo iwaokowe wafungwa Sheikh Namer na Alamah Al-Amiriy na wanasiasa wote ndani ya Saudia Arabia ili kulinda na kuhifadhi haki za binadamu, kuwapa Mashia haki, uhuru wa kushiriki katika kila nyanja nchini humo.

2013/03/30  10:23

Muamko wa Kiislamu
Kupigwa vibaya mkazi wa Bahrain na kuonyesha unyama wa utawala wa Alikhalifa+picha
Alkhamis ilitolewa ripoti na Chama cha Alwifaq Bahrain kulingana na ukandamizaji wa utawala huo dhidi ya Wananchi ambao waandamana kwa amani kuhitaji wakubaliwe maombi yao, katika maeneo ya Almarakh waliandamana Wananchi maandamano ya amani ila jibu lao lilikuwa ni kupigwa vibaya kupelekwa Hospitali na baadhi kuaga maisha yao.

2013/03/30  10:16

Korea kaskazini na Marekani
Kim Jong-un kuandaa jeshi lake dhidi ya vita na Marekani
Rais Kim Jong-un wa Korea Kaskazini leo asubuhi ameitisha mkutano wa dharura wa wakuu wa jeshi la nchi hiyo na kuagiza jeshi liko tayari kurusha makombora yake ya kimkakati ili kushambulia kambi za kijeshi za Marekani zilizoko eneo la kivita la Pasifiki kwa wakati wowote.

2013/03/29  23:58

Hatima ya upinzani Syria
Riadh Al-Asad yupo hai+ picha ya mguu ulokatwa
Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Siku ilopita tarehe 25/3/2013, Riadh Al-Asad Mkuu wa waasi wa Syria almaarufu kama jeshi huru la Syria kajeruhiwa vibaya ndani ya nchi hiyo na kusababisha kuzagazwa habari tofauti kunako kamanda huyo wa jeshi. Ama picha hii yaonyesha kuwa yupo hai ila hana mguu mmoja kwa athari ya mrupuko, aidha aoneka kuwa na majeraha mengi, kwa sasa kamanda huyo alisafirishwa Uturuki kwa ajili ya matibabu.

2013/03/27  00:16

AFRIKA
Mubarak aachiwa huru tarehe 14/4/2013
Mwanasheria mkuu nchini Misri atangaza kuachwa huru Husni Mubarak 14 mwezi wa nne

2013/03/26  22:35

Facebook na Twiter hutumika kusaidia majasusi wa Marekani
muasisi wa mtandao wa WikiLeaks Julian Assange ambaye sasa yuko mafichoni London katika mazungumzo ya siri na waandishi wa habari alielezea kuwa:

2013/03/26  14:09

Hatima ya upinzani Syria
Jeshi huru la Syria kutomtambua rasmi Ghassan Hitto
Jeshi huru la Syria limeeleza kuwa halimtambuwi Ghassan Hitto kuwa rais wa muda wa Muungano wa Upinzani Syria.

2013/03/25  02:34

Hatima ya upinzani Syria
Muadh Khatib kajiuzulu kwa uzembe wa Jumuiya za Kimataifa
Ofisi rasmi ya Ahmad Muadh Khatib imeeleza kuwa sababu ya kujiuzulu kiongozi huyo ni kuzembea Jumuiya za Kimataifa katika baadhi ya mambo.

2013/03/25  02:27

Habari za Syria
Kuundwa serikali ya muda na hitilafu za ndani ndio sababu kuu ya kujiuzulu Khatib
Mmoja wa viongozi wa wapinzani syria ambae aishi nje ya Syria alieleza kua sababu kuu ya kujiuzulu Muadh Khatib ni hitilafu za ndini wapinzani na kuteuliwa Waziri Mkuu wa wapinzani wa Syria.

2013/03/25  02:24

Habari za Syria
Muungano wa upinzani wa Syria kukataa kujiuzulu Muadh Khatib
Muungano wa upinzani wa Syria umeeleza kuwa kujiuzulu kwa kiongozi huyo hakukubali na yeye bado ahisabika ni rais wa umoja huo.

2013/03/25  02:15

Habari za Syria
Muadh Khatib kujiengua madarakani
Rais wa wapinzani Syria ajiuzulu na kuandika katika ukurasa wake wa Facebook: Mimi niliwaahidi wasyria nachukua cheo hiki kwa masharti na ikivukwa misitari myekundu nitajiuzulu.

2013/03/25  02:08

Afrika
Kikundi cha Ikhwanul Muslimina nchini Misri si cha kisheria tena
Kamati inayo fungamana na mahakama kuu ya Misri imetangaza kuwa hukumu ya kunyimwa kibali kikundi cha Ikhwanul Muslimina iliotolewa mwaka 1992 ni hukumu halali na sahihi

2013/03/22  22:26

Baada ya Hugo Chavez
Venezuela yataka mahusiano na mwanadiplomasia wa Marekani
Baada ya ya Hugo Chavez nchi ya Venezuela kuingia katika duru mpya ya kisiasa kuanza kufukuza kila mwanadiplomasia wa Kimarekani nchini humo.

2013/03/22  01:41

Afrika
Kaka wa Gadafi akamatwa nchini Misri
Mtoto wa baba mdogo wa dikteta wa zamani wa Libya Gaddafi ajisalimisha baada ya kuzingirwa nyumbani kwake na jeshi la ulinzi nchini Misri

2013/03/21  22:14

Uturuki na washiriki wake kufeli kunako mgogoro wa Syria
Silaha za kikemia kutumiwa na waasi Syria
Shirika la habari la Syria limetangaza kuwa magaidi wamefyatua silaha za kikemia katika eneo la Khan al-Assal katika mkoa wa Aleppo, na waziri wa habari Omran al-Zohbi amesema mashambulizi hayo yanazusha hali ya hatari. Naibu waziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi hiyo Faisal Muqdad amesema kuwa watu 31 wameuawa katika mashambulizi hayo, ambayo pia yamewajeruhi wengine zaidi ya 100.

2013/03/21  01:42

Ulaya na Cyprus
Wasi wasi wa viongozi wa Ulaya kunako kura ya Cyprus
Rais wa Cyprus Nicos Anastasiades anakutana na viongozi wa vyama vya kisiasa katika hatua ya dharura ya kutafuta mpango mbadala baada ya bunge kukataa mpango wa Umoja wa Ulaya wa uokozi.

2013/03/21  01:02

Mashariki ya kati
Watu 20 wauawa na wengine 97 wajeruhiwa katika mashambulizi ya mabomu nchini Iraq
Watu 20 wameuawa na zaidi ya 97 kujeruhiwa katika mfululizo wa milipuko ya mabomu na risasi nchini Iraq mapema leo.

2013/03/19  23:57

Habari muhimu
Wafungwa 1059 kuachiwa huru kwa hukumu ya kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya Kiislamu
Kukaribia Idi na mwaka mpya Iran kiongozi muadhamu wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran asamahe wafungwa 1059 na zaidi ya wafungwa alfu 59 kupunguziwa kifungo chao.

2013/03/19  16:25

Uwahabi ni hatari
Utawala wa Ali Saudi kuharibu athari za Kiislamu kwa madai ya marekebisho
Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Gazeti moja la Saudia Arabia limeeleza kua utawala wa Ali Saudi umeanza opresheni zake za kuharibu athari za Kiislamu katika mji wa Mak`kah kwa madai ya marekebisho na kupanua Masjid Al-Haram, na marekebisho hayo ya gharimu zaidi mabilioni dola, urekebishaji huo ulianzia kwenye baadhi ya sehemu za kihistoria ambazo hapo kabla haikukubaliwa kuvunjwa kwa ajili ya marekebisho. Kuharibu sehemu kwa marekebisho hakuna mushkili ila ilsiwe sehemu za kihistoria ambazo Waislamu hujikumbusha na kuleta kumbukumbu za zama za Mtukufu Mtume(saw), ipo wazi Mawahabi kila siku hujitadi kuharibu na kuvunja sehemu za kihistoria kwa madai ya kua kuacha athari hizo za kihistoria husababisha kuzidi shirki ya Mwenyezi Mungu.

2013/03/19  15:50

Silaha ni hatari kwa jamii
Mataifa kujadili udhibiti wa biashara ya silaha
Wawakilishi kutoka mataifa 150 wanakutana leo mjini New York Marekani, katika shinikizo la mwisho la kuunda mkataba wa kimataifa, unoalenga kukomesha uuzaji wa silaha kiholela, lakini Marekani inashinikizwa kuukataa.

2013/03/18  00:01

Mgogoro wa Syria
Mgogoro wa Syria kuchochewa zaidi na kupewa waasi silaha na mafunzo
Kituo cha Habari cha Marekani CNN kimesema, mamia ya wapiganaji waasi wa Syria wamepewa mafunzo kwa kutumia silaha za kisasa. Mafunzo hayo yameandaliwa na kupitishwa na Marekani katika kambi moja iliyopo nchini Jordan.

2013/03/18  16:17

Habari za Iran
Iran yatuma manowari ya kivita katika bahari ya Caspian kulinda usalama wa ukanda huo
Iran kuonyesha ulimwengu iko tayari kulinda maslahi ya kila nchi kutuma manowari za kivita katika bahari ya Caspian, yote hayo ni kuonyesha sura kamili ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran.

2013/03/18  15:56

Maafa ya mwaka 2012 duniani yaleta hasara zaidi ya bilioni 100 za dola za kimarekani
Shirika la kukabiliana na maafa ya dunia la Umoja wa Mataifa(UNISDR) limesema, hasara iliyotokana na maafa yaliyotokea duniani kwa mwaka jana imefikia dola za kimarekani bilioni 138.

2013/03/16  20:22

Amerika
Maduro kuapishwa kuwa rais wa muda wa Venezuela
Makamu wa rais wa Venezuela, Nicolas Maduro, anatarajiwa kuapishwa leo kuwa rais wa muda wa nchi hiyo. Hayo yamesemwa jana na Spika wa bunge la Venezuela, Diosdado Cabello.

2013/03/10  11:46

Amerika
Rais Hugo Chávez afariki dunia
Rais wa Venezuela Hugo Chávez amefariki dunia jana tarehe 5 mwezi wa tatu mwaka huu wa 2013.

2013/03/06  08:13


         10  11  12  13  14  15  16  17  18  19  20  
ABNA World Service
Englishالعربية
Françaisاردو
Españolفارسی
Русский中文
DeutschTürkçe
Azeri (cyr) Azeri (ltin)
Melayu Indonesia
বাংলা हिन्दी
Swahili Myanmar
BosanskiABP sites
  Habari za Zamani