Abna.ir


Iran yalaani ukatili wa utawala wa Bahrain
Ukatili Bahrain
Iran yalaani ukatili wa utawala wa Bahrain

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani mauaji ya kijana moja huko Bahrain katika Siku Kuu ya Idul Fitr na kuelezea wasi wasi wake kuhusu kuendelea kuwepo vikosi vya kigeni katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi.

Ripoti ya Shirika la Habari la Ahlul Bait(a.s)-ABNA-Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani mauaji ya kijana moja huko Bahrain katika Siku Kuu ya Idul Fitr na kuelezea wasi wasi wake kuhusu kuendelea kuwepo vikosi vya kigeni katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Ramin Mehmanparast ameongeza kuwa vikosi vya kigeni nchini Bahrain ni kizingiti katika kurejea utulivu nchini humo.
Siku ya Jumatano vikosi Bahrain vinavyopata himaya ya vikosi vya Saudi Arabia vilimuua shahidi Ali Jawad Ahmad al Sheikh aliyekuwa na umri wa miaka 14 kwa kumpiga risasi usoni. Kijana huyo aliuawa katika maandamano ya baada ya Sala ya Idul Fitr katika mji wa Sitra. Hospitali ya mji huyo, chini ya mashinikizo ya serikali, ilikataa kumtibu kijana huyo ambaye aliaga dunia kutokana na majeraha aliyopata.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, ‘hakuna mantiki inayoweza kuhalalisha kuuawa shahidi kijana huyo wa Bahrain katika idi kubwa ya Waislamu'. Ametoa wito kwa serikali ya Bahrain kutumia njia za busara na uadilifu ili utulivu urejee nchini humo.



http://www.abna.ir/data.asp?lang=17&id=263262