Abna.ir


Jannati: Iran haitosimamisha miradi yake ya nyuklia hata kwa lahadha moja
Jannati: Iran haitosimamisha miradi yake ya nyuklia hata kwa lahadha moja

Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, taifa la Iran halitosimamisha miradi yake ya nyuklia hata kwa lahadha moja.

Ayatullah Ahmad Jannati amesema hayo mbele ya hadhara ya waumini waliohudhuria ibada ya Sala ya Ijumaa na kuwatahadharisha wananchi wa Misri na Yemen wawe macho na njama za maadui. Ayatullah Jannati amesema, Marekani ndilo dola la kwanza lililopatikana na hatia kwa kutumia silaha za mauaji ya umati na kusisitiza kwamba, kutokana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa na himaya na uungaji mkono mkubwa wa wananchi haina haja ya kuwa na silaha za nyuklia.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran ameitaka Marekani na washirika wake kutambua kwamba, Iran sio taifa la kulipigisha magoti kupitia vitisho, mashinikizo na vikwazo; kwani taifa hili limesimama kidete na katu halitalegeze kamba hata kidogo kuhusiana na suala la miradi yake ya nyuklia inayofanyika kwa malengo ya amani.


http://www.abna.ir/data.asp?lang=17&id=280537