Muamko wa Kiislamu Kuachiwa huru Mwanamke wa Kibahrain baada ya kifungo cha mwaka mmoja A`ayat Hasan Qarmazit mwenye Umri wa miaka 20 Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mafunzo na Malezi na Mshairi wa mapinduzi ya Bahrain kuachiwa huru. |
Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- A`ayat Hasan Qarmaziy alishikwa tarehe 14 February 2011 kwa kosa la kutunga na soma shairi lake hadhani na kutangaza uadui wake na utawala wa Alikhalifa, Mwanamke huyu alitiwa mbaroni siku ya Jumatano tarehe 30 March 2011, na tarehe 20 April 2011 ilitangazwa kifo chake na utawala wa Alikhalifa Bahrain na vyombo vya habari vilitangaza habari ya Shahada yake, ila Mama A`ayat alikanusha suala hilo na mara kadhaa aliongea na Shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA-kwa Telephone kueleza kuwa mwanae bado yupo hai na kila siku waongea kwa njia ya Simu.
Nabiil Rajab Kiongozi wa haki za Binadamu Bahrain alisema: habari za kuuawa A`ayat HasanQarmaziy ni propaganda za utawala kifalme Bahrain na hazina uhakika ndani yake.
Habari ya kuhukumiwa A`ayat Hasan Qarmazit ilitolewa tarehe 12 June 2011 kuhukumiwa mwaka mmoja, na mnamo siku ya Jumatano Saa 17:30 kwa muda wa Bahrain iliachiwa huru kwa masharti baada ya kukaa Jela siku 100 kuteswa kimwili sasa kawa huru, na kuachwa kwake huru Familia yake ilimpokea kwa shangwe na vigeregere wakiwa pamoja na wanamapinduzi wa Bahrain.http://www.abna.ir/data.asp?lang=17&id=299449